Watuhumiwa wengine wa wizi wa pesa ya EPA wamefikishwa mahakama ya Kisutu jana huku kukiwa na tetesi miongoni mwa watanzania kwamba wanaofikishwa kotini siyo wezi halali wa pesa hizo kutoka Benki kuu ya Tanzania.
Wananchi wengi waliotoa maoni yao wanabeza uamuzi huo wakisema kwamba hatua hiyo aina nguvu kwa sababu watuhuhumiwa wazito wameachwa na wanaopelekwa huko ni 'mchezo wa maigizo'
"Kwa maoni yangu sijaridhika, hatua hiyo haina chochote. Nilitaka kuona full list, siyo hawa wachache tena wadogo" anasema Dr. Wilbroad Slaa, Katibu Mkuu wa Chadema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment