Monday, November 17, 2008

Malecela: Walimu walipwe haraka.

Mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa Mtera John Malecela ameitaka serikali ilipe haraka madai ya walimu ili kuzuia usumbufu unaoweza kujitokeza usio na msingi aliyasema hayo jana kutoka Dodoma.

“Ili kusiwe na athari yoyote kwa watoto wetu serikali inapaswa kukaa na kuweka mikakati madhubuti ya kudumu kuwalinda watoto wetu wasihathirike wakati walimu wanapokuwa katika migomo kama hii” alisema

Taarifa ya Malecela inatokana na mgomo wa walimu nchi nzima ulioanza leo kuishinikiza serikali iwalipe walimu madai mbalimbali.

Akitoa taarifa ya mgomo nchi nzima Raisi wa Chama cha walimu, Gratian Mkoba alisema kwamba serikali imeshindwa kuwalipa walimu madai yao na kumekuwepo kauli za kupotosha umma kutoka kwa viongozi wa serikali kuhusu madai yao.

“Nawasii walimu wote wasitishike na vitisho vya aina yoyote ile kwani mgomo umeandaliwa kisheria na kukamilisha taratibu zote za kisheria” alisema.



Vigogo wa EPA Kufikishwa mahakamani.

Kuna taarifa za siri kwamba baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali ya Kikwete na wa serikali ya awamu ya tatu ya Benjamini Mkapa wanaweza kufiikishwa mahakamani kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu kutoka Benki Kuu.

“Kuna orodha ndefu ya vigogo na Waziri mmoja aliyekuwemo katika baraza la Kikwete kabla alijavunjwa kutokana na kashfa ya Richmond” chanzo cha habari kilisema.

Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti mmoja la kila wiki kuna tetesi kwamba Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma (DPP) anaendelea na upelelezi zaidi kwa majalada ya vigogo hao kwa tuhuma za ufisadi.

No comments: