Saturday, November 15, 2008

Walimu Tanzania kugoma nchi nzima Jumatatu.

Mahakama YA RUFAA imebatilisha uamuzi wa MAHAKAMA ya Kazi kuhusu mgomo wa walimu na kutoa kibari cha kuruhusu mgomo huo kufanyika nchi nzima Jumatatu.

Rais wa CWT Gration Mkoba amesema walimu wamepata haki yao ya msingi na wasiingie madarasani hadi hapo serikali itakapowapatia madai yao yote

“Sasa walimu watagoma na pengine tutakutana na serikali mwezi Januari” amesema

Otoba 13 Jaji wa Mahakama ya Kazi Wlliamu Mandia alitoa kibari cha kuzuia mgomo kwa maelezo kuwa ungeathiri sekta nzima ya elimu hasa wnafunzi wa kidato cha nne amabao walikuwa wakiendelea na mitihani ya kumaliza elimu ya sekondari.



Watuhumiwa wa EPA wafanya maajabu.

Watuhumiwa Johnson Mwesiga Lukaza na wenzake wa Kampuni ya Kernel Limited Ijumaa waliachwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana lakini waliondoka mahakamani katika njia ya ajabu.

Walitumia ujanja wa kumtanguliza mmoja wa ndugu yao aliyetangulia kwa kunyoosha mikono juu kushangilia kana kwamba ndiye aliyeachwa huru huku wao wakipita njia nyingine kuwakimbia waandishi wa habari.

Waandishi wa habari za picha walipofuatilia waligundua kwamba siye aliyeachwa huru huku watuhumiwa wenyewe wakiwa wameishapanda gari na kuondoka aina ya Suzuki Escudo.
Maziwa yaliyokutwa na mealmine Dar es salaamKulia, Raymond Wigenge, Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula, Kushoto, Ms Charis Ugullum, Mkurugenzi huduma za maabara wa Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA)